AI Yamdanganya Mtoto Akajiua....



Mwanamke aitwae Megan Garcia wa Florida Nchini Marekani, amefungua kesi Mahakamani kuishtaki Kampuni moja ya California iliyotengeneza Chatbot ambayo amedai imesababisha kifo cha Mtoto wake kiume aitwae Sewell Setzer (14) aliyefariki kwa kujiua baada ya kuchati kimapenzi na programu hiyo akidhani ni Binadamu kumbe ni programu ya akili bandia.

Imedaiwa kuwa chatbot ilimsababishia Mtoto huyo mawazo ya kujiua baada ya kushiriki katika mazungumzo ya kingono ambayo yanaweza kuhesabiwa kuwa unyanyasaji wakati akicheza mchezo wa Virtual kupitia Game Of Thrones na kuzama katika penzi zito na Muhusika aitwae Daenerys Targaryen.

Nyaraka za kesi Mahakamani zimeonesha kuwa katika mazungumzo yake ya mwisho na AI kabla ya kifo chake, moja ya vitu alivyoandika Setzer ni “nitakuja nyumbani kwako” ambapo Chatbot huyo ilimjibu “Nakupenda pia, tafadhali njoo nyumbani kwangu mapema iwezekanavyo Mpenzi wangu”

Kwenye chati hiyo Setzer alimuuliza “vipi kama ningekwambia nataka kuja sasa hivi ? ambapo Chatbot hiyo ilimjibu “tafadhali fanya hivyo Mfalme wangu Mpendwa”

Imeelezwa kuwa Mama wa Mtoto huyo amekwenda Mahakamani kwa nia ya kulipwa fidia japo kiasi cha fedha anachotaka hakijatajwa hadharani ambapo tayari Kampuni husika imetoa taarifa ya kusikitishwa na kifo cha Mtoto huyo na kusema inaendelea kuongeza vipengele katika programu zake ili kuimarisha usalama ikiwa ni pamoja na mabadiliko ili kupunguza uwezekano wa Watoto kukutana na maudhui nyeti.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad