Aitana Bonmatí Ashinda Tuzo ya Mchezaji Bora Duniania Kwa Wanawake Ballon d’Or Féminin



Kiungo wa Klabu ya Wanawake ya Barcelona na Timu ya Taifa ya Uhispania, Aitana Bonmatí Conca (26) ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia kwa upande wa wanawake inayojulilana kama Ballon d’Or Féminin.

Bonmati ambaye mpaka sasa katika Ligi Kuu ya soka la wanawake ana magoli 3 katika michezo mitano aliiongoza Timu ya Uhispania kutwaa taji la UEFA Women’s Nations League mwaka 2024 na alifanikiwa kutwaa tuzo ya mwanamichezo bora mwanamke ya Laures World Sport.

Bonmati ametwaa tuzo hiyo kwa kuwashinda wapinzani wake kama Caroline Graham Hansen (29) raia wa Norway na klabu ya Barcelona pamoja na Mallory Swanson (26) kutoka Marekani anaechezea Chicago Red Stars.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad