Aliemshtaki Diddy Alitoa Hongo ya Bilioni 8.1

Aliemshtaki Diddy Alitoa Hongo ya Bilioni 8.1


Mwanamke aliyemshtaki Diddy anadaiwa kujaribu kumhonga aliyekuwa mpenzi wake kwa dola milioni 3 sawa na Tsh bilion 8.1ili kumuunga mkono kwenye madai yake


Thalia Graves ambaye hivi karibuni alifungua kesi akimtuhumu Diddy kwa ubakaji na kurekodi kitendo hicho, sasa anadaiwa kujaribu kumhonga mpenzi wake wa zamani na ofa ili kuunga mkono madai yake.


Kwa mujibu wa TMZ imepata meseji zinazoonyesha kwamba Graves alikuwa tayari kulipa dola milioni 3 ambazo ni sawa na Tsh bilion 8.1 kwa mpenzi wake wa zamani ikiwa angekubali kuthibitisha hadithi yake mahakamani.


Kesi hiyo iliyofunguliwa dhidi ya #Diddy na mkuu wake wa zamani wa usalama, Joseph "Big Joe" Sherman, inadai kuwa Graves alibakwa na nguli huyo wa muziki mwaka 2001. Graves anadai mpenzi wake wa wakati huo ambaye alikuwa akifanya kazi kwa Diddy wakati huo, alionyeshwa rekodi ya tukio linalodaiwa.


Sasa yamepatikana yanayoonyesha mazungumzo kati ya Graves na ex wake mnamo Novemba 2023 kuonyesha upande tofauti wa hadithi.


Kwa mujibu wa maandishi hayo, Graves alisema waziwazi kwamba ana mpango wa kumshtaki Diddy "kwa sababu yeye ndiye mwenye pesa." Kisha inasemekana alimpa mwanamume huyo pesa hizo ili kutoa ushahidi kwamba alikuwa ameona video inayodaiwa kuonyesha tukio


Katika moja ya maandishi, Graves anaonekana kumuuliza ex wake moja kwa moja. "Unafikiri nini kuhusu $3 mil?" baada ya kujadili kesi hiyo. Mwanamume huyo, ambaye anasema alitafsiri ujumbe huo kama jaribio la kumhonga ili kuunga mkono shutuma zake.


Alieleza kuwa baada ya kupokea ujumbe huo, alimzuia mara moja na kukata mawasiliano. Wakati huohuo, timu ya wanasheria wa Diddy imeripotiwa kupata nakala za jumbe hizo hizo zilizopatikana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad