Aliyetishia Kuua Kwa Bastola Dar Afikishwa Mahakamani, Akana



Mshtakiwa aliyetajwa na hati ya Mahakama kwa jina la Derick Derick Junior (36) amefikishwa katika Mahakama ya Kinondoni Jijini Dar es salaam leo akikabiliwa na mashtaka mawili ikiwemo kutishia kwa silaha ikiwa ni baada ya kusambaa kwa video yake akionekana kumjeruhi Mtu kwa kumpiga na kitako cha bastola.

Mshtakiwa huyo amefikishwa Mahakamani hapo leo na kusomewa mashtaka yake na Wakili wa Serikali, Dickson Swai mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Hakimu Mfawidhi Is-haq Kuppa huku pia Mtu aliyejeruhiwa akifika Mahakamani hapo kufuatilia mwenendo wa kesi hiyo.

Imedaiwa kuwa Mshtakiwa Derick alitenda makosa hayo Oktoba 27, 2024 nje ya Club ya usiku ya ‘1245’ iliyopo Masaki, Kinondoni Jijini Dar es salaam ambapo alimjeruhi Mtu aitwae Julian Bujulu kwa kumpiga na kitako cha bastola na kumjeruhi sehemu ya jicho na pua.

Baada ya Mshtakiwa kusomewa mashtaka yake alikana makosa hayo na kutimiza masharti ya dhamana ya kutakiwa kuwa na Mdhamini ambaye ni Mtumishi wa umma atakayesaini bondi ya shilingi milioni nane ambapo aliyatimiza na kuachiwa kwa dhamana huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi November 20, 2024 itakapoitwa tena kwa ajili ya kutajwa.

Julian Bujulu pekee ndiye aliyenaswa na camera za Waandishi wa habari baada ya Derick kufanikiwa kuwakwepa Waandishi Mahakamani hapo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad