Tumezoea kuimba ngojera za kuonyana kuhusu Rwanda, Burundi na Somalia kwamba hawana amani sababu ya vurugu tunazowatungia ili kunyimana uhuru.
Natamani tuanze kuiimba Kenya kama “shamba darasa” la siasa na “ukatiba” katika ukanda wetu wa Afrika Mashariki na Kati. Nimejifunza yafuatayo toka shamba darasa hilo:
1. Kuna tofauti kati ya Deputy President na Vice President. Mmoja kati ya hao aweza kuishi bila kusema “shikamo Mheshimiwa Rais” na mwingine aweza kuacha kwa hasara yake mwenyewe.
2. “Vitengo” vyote vinafanana kote. Ukimwaga mboga ya kitengo, chenyewe kinamwaga ugali wako. Rigy G alimpiga kiwiko DG wa Kitengo. Haya yaweza kuwa matokeo.
3. Kama Kitengo kimemsaidia Ruto, basi na yeye shingo iko Kibra. Achague moja; ama kuwa mtumwa wa kitengo milele au ajiandae kunyolewa. Ukiona shamba boy anamwagiza mama mwenye nyumba amletee maji ya kunywa ujue “kwisa habari yake”.
3. Tanzania tuna katiba, Kenya wana “ukatiba”. Tofauti yake utaijua ukionja. Ukatiba ni sumu ya watawala. Katiba ni sumu ya wananchi. Tunahitaji daraja kutoka katiba kwenda ukatiba. Mgombea binafsi ni daraja la gharama ndogo.
4. Bila ukatiba, wananchi na watawala hawako salama; Maendeleo ya watu ni ndoto. Maendeleo ya vitu yako hatarini kuharibiwa na watu wasio na maendeleo.
5. Elimu ya Kenya imeonyesha ubora wake kupitia wanasheria. Utadhani akina Marando, Kanywani, Shivji, Lamwai, Ringo Tenga, El-Maamry na Ndyanabo walihamia Kenya. Elimu yetu ya Sheria inafundisha watu kulinga, kufoka na kubet. Natamani wanasheria wetu waone wivu.
6. Gen Z hawajamalizana na Ruto. Rigy G hajamalizana na Ruto. “Mlima” haujamalizana na Ruto. Mahakama haijamaliza na Ruto. Uhuru hajamalizana na Ruto. Na Ruto huyu hajamalizana na Ruto yule.
Wanyambo wanasema STAY TUNED.