Bacca Awashusha Presha Mashabiki Yanga

Bacca Awashusha Presha Mashabiki Yanga

 Bacca Awashusha Presha Mashabiki Yanga

Hali ya beki wa kati wa Yanga, Ibrahim Abdallah 'Bacca' ni nzuri na mlinzi huyo atacheza mechi dhidi ya watani zao, Simba itakayochezwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, imeelezwa.


Yanga imelazimika kutoa kauli hiyo kufuatia tetesi huenda Bacca akaukosa mchezo huo kwa sababu ni majeruhi.


Meneja wa Yanga, Walter Harrison, alisema jana mchezaji pekee ambaye ni majeruhi katika kikosi chao ni Farid Mussa lakini ameshaanza mazoezi maalum ya kurejesha utimamu wa mwili, kabla ya kujumuika pamoja na wenzake.


"Hakuna taarifa yoyote ya majeruhi, na wachezaji wote waliokuwa kwenye vikosi vya timu za taifa, wameshawasili, hakuna yoyote aliyerejea akiwa na majeraha, mtu pekee ambaye bado na matatizo ni Farid, na yeye pia ameshaanza mazoezi mepesi ili kurudisha utimamu wa mwili kabla ya kujiunga na wenzake.


Nasema hakuna taarifa yoyote nyingine ya upande wa majeraha ya wachezaji wetu, kikosi chetu kiko imara na tayari kwa dabi hiyo," Harrison alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad