Mastraika Prince Dube na Jean Baleke wameanza kuzua wasiwasi ndani ya klabu ya Yanga baada ya kushindwa kuanza msimu vizuri.
Dube aliyejiunga na Yanga kama mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Azam FC, alianza vizuri katika mechi za kujiandaa na msimu pamoja na zile za CAF lakini ameshindwa kabisa kuonyesha makali hayo kwenye Ligi.
Kwa upande wa Baleke ameshindwa kabisa kumshawishi Kocha Miguel Gamondi kumpanga katika kikosi cha kwanza hivyo kupata dakika chache tu za kucheza.
Mastraika hao wawili ambao wamewahi kufanya makubwa na Azam FC na Simba, wameibua maswali juu ya Nini ambacho kinawafanya washindwe kutamba na Yanga.
Inaelezwa kuwa Kocha Gamondi anaridhishwa zaidi na kiwango cha Clement Mzize na ndio kipaumbele kwake katika kikosi cha kwanza.