BREAKING: Hatimaye Boniface Jacob Aachiwa Huru Kwa Dhamana

BREAKING: Hatimaye Boniface Jacob Aachiwa Huru Kwa Dhamana


BREAKING: Hatimaye Boniface Jacob Aachiwa Huru Kwa Dhamana


Leo, Jumatatu Oktoba 07.2024 Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu imekubaliana na hoja za utetezi kuhusu pingamizi la kutopatiwa dhamana lililokuwa limewekwa na Jamhuri/ serikali dhidi ya aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kinondoni na baadaye Ubungo, Dar es Salaam Boniface Jacob (Boni Yai), hivyo mwanasiasa huyo amepatiwa dhamana inayoendana na masharti yatakayowekwa kwenye shauri la msingi, ambalo sasa linaendelea

Maamuzi hayo madogo ndani ya kesi ya msingi yametangazwa Mahakamani hapo na Hakimu mkazi Mkuu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam ambapo shauri hilo lililetwa Mahakamani hapo kwa ajili ya kusomwa hukumu ya kesi ndogo ndani ya kesi ya msingi;

Jambo TV itaendelea kukupatia taarifa zaidi kuhusiana na kile kilichojitokeza Mahakamani hapo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad