BREAKING: Mtangazaji Dida Shaibu wa Wasafi FM Afariki Dunia

 

BREAKING: Mtangazaji Dida Shaibu wa Wasafu FM Afariki Dunia

Mtangazaji wa Wasafi FM kupitia kipindi cha 'Mashamsham', Khadija Shaibu maarufu kama Dida amefariki Dunia usiku huu wa leo Ijumaa, Oktoba 4, 2024 baada ya kuugua na kulazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa za msiba huo zimethibitishwa na mtangazaji mwenzake, Maulid Baraka Kitenge kupitia mitandao yake ya kijamii.

Kitenge ameandika; “Dida shaibu wa Wasafi FM amefariki dunia."

Didah amefikwa na umauti akiwa na umri wa miaka 42, ambapo kifo chake kimetokea siku kumi na sita (16) toka Wafuasi wake washuhudie ukimya wake katika mitandao ya kijamii ambapo chapisho lake la mwisho mtandaoni lilikuwa Septemba 19, 2024 ambapo aliweka picha yake akiwa kwenye gari ikisindikizwa na wimbo wa Martha Mwaipaja “Amenitengeneza".

Kabla ya kutua Wasafi, Dida alikuwa akifanya kazi ya utangazaji katika kituo cha Times FM kupitia kipindi cha Mirindimo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad