BREAKING: Mtoto Joel Aliyepotea Mlimani Arusha Apatikana

BREAKING: Mtoto Joel Aliyepotea Mlimani Arusha Apatikana

BREAKING: Mtoto Joel Aliyepotea Mlimani Arusha Apatikana

Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Bagara, Joel Mariki, aliyedaiwa kupotea tangu Septemba 14, 2024 eneo la Mlima Kwaraa mjini Babati mkoani Manyara, ambapo alikwenda kufanya mafunzo kwa vitendo na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, amekutwa katika eneo la Galapo na msamaria mwema aliyemfikisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, akiwa na majeraha katika mwili wake huku akiwa amedhoofika kwa kutokula kwa muda mrefu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Catherine Magali, amethibitisha kumpokea mtoto huyo hospitalini hapo.

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga, amefika hospitalini hapo na kumjulia hali mtoto huyo kisha akazungumza na wanahabari ambao hawakuweza kupata picha za mtoto huyo ambaye yupo kwenye uangalizi wa karibu na madaktari.

Baba mzazi wa kijana huyo ameeleza furaha yake baada ya kumpata kijana wake akiwa hai.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad