Dereva wa Basi la Asante Rabi Aliyesababisha Ajali na Kuuwa Watu 4 Akamatwa



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilibroad Mutafungwa.

JESHI la Polisi mkoani Mwanza limethibitisha kumkamata Shadrack Michael Swai (37) Mkazi wa Arusha ambaye ni Dereva wa basi lenye namba za usajili T-458 DYD aina YUTONG mali ya kampuni ya Asante Rabi linatajwa kusababisha ajali iliyotokea wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kusababisha vifo vya watu wanane na majeruhi 39.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza DCP Wilibroad Mutafungwa amethitisha kumatwa kwa Dereva huyo jioni ya Oktoba 22 na kueleza kuwa baada ya tukio alitokomea kusikojulikana.

"Swahi anakabiliwa na kosa la kuendesha gari kwa uzembe na kushindwa kuchukua tahadhari na kusababisha ajali iliyoleta vifo na majeruhi,"amesema DCP Mutafungwa.

DCP Mutafungwa amesema ajali hiyo imetokea Oktoba 22, 2024 majira 06:10hrs katika Barabara ya Mwanza - Shinyanga eneo la kijiji cha Ngudama Tarafa ya Usagara wilaya ya Misungwi mkoa wa Mwanza.

Amesema gari lenye namba za usajili T458 DYD kampuni ya Asante Rabi ikitokea Mwanza kuelekea Arusha likiendeshwa na Shadrack Swai lilihama upande wake na kugongana na gari lenye namba za usajili T.281 EFG aina ya YUTONG BUS kampuni ya Nyehunge iliyokuwa ikitokea Morogoro kuelekea Mwanza.


Amesema ajali hiyo imesababisha vifo vya watu wanane, ambapo watu watano watano wamefariki kwenye eneo la ajali na watatu watatu wamefariki wakiwa wanapatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Misungwi.

Amesema Waliofariki katika ajali hiyo wanne wametambuliwa kwa majina ambao ni Zamda Darius(30), Mkazi wa Usagara, Jacob Elius(43), Mkazi wa Chibe Shinyanga, Godluck Mshana (18), Edward Lazaro(20), mkazi wa Shirati.


Aidha amesema miili ya watu wanne bado haijatambuliwa na inaendelea kuhifadhiwa katika Hospital ya Wilaya ya Misungwi.

Amesema Majeruhi wanaoendelea na matibabu katika hospital ya Rufani Kanda Bugando ni Doricas Joseph (38), mkazi wa Mkuyuni, Shija Kazori(41), Mkazi wa Mabatini, Magreth Hardson(31), Mkazi wa Mecco, Isack Daud(28), Amani Adrew(27), Mkazi wa Bugarika, Silivia Sita(28), Mkazi wa Mkuyuni, Janeth Mathias (26), Mkazi wa Geita.

Aidha kupitia mtandao wake wa WhatsApp Rais Samia Suluhu Hassan amesema "Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali za barabarani zilizotokea katika mikoa ya Mwanza na Kilimanjaro na kusababisha vifo na majeruhi. Nawapa pole wafiwa wote, familia, ndugu, jamaa na marafiki. Nawaombea marehemu wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka".


"Tunapoelekea mwishoni mwa mwaka, nawasihi watumiaji wote wa barabara kuongeza umakini. Nimeziagiza mamlaka zote husika kuongeza umakini katika usimamizi wa sheria za usalama barabarani," amesema Rais Samia

"Mwenyezi Mungu azilaze roho za ndugu zetu hawa mahali pema peponi. Amina." amesema katika Mtandao wake wa WhatsApp.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad