Dudu Baya Atoa Mpya: Monalisa Alikuwa Mpenzi Wangu, Nilimkosea sana

 

Dudu Baya Atoa Mpya: Monalisa Alikuwa Mpenzi Wangu, Nilimkosea sana

Msanii wazamani wamuziki wa bongo fleva Godfrey Tumaini maarufu kama Dudu Baya, Mamba, konkimansta, akiwa kwenye maojiano na mtangazaji wa habari ameweka wazi kuwa mwanadada Monalisa amewaikuwa mpenzi wake na walipendana sana.


“Hakuna mwanamke nampenda mpaka leo kama Monalisa. Jinsi tulivyokuwa tunapendana, hata tukikutana naye usoni hivi hatakagi kuniona kwa sababu tukionana hivi tu atashawishika niondoke naye.


“Monalisa alinipenda sana na nilimkosea kwa sababu wakati nimekwenda kusoma Nairobi mwaka 2003, nikakutana na mwanachuo mwenzangu ambaye ni Mkenya anaitwa Banis. Nilipoanza naye mahusiano.


“Tukiwa sebureni na Monalisa, Banis akanipigia simu anataka matumizi, nilichokosea nikamtumia pesa, Monalisa alinimaindi hapo hapo, kwa hiyo nilimchiti, Monalisa nisamehe.


“Kwa sasa namheshimu, sijui yuko na nani, naheshimu watoto wake, sina mawasiliano naye. Monalisa anajua tunavyopendana lakini ninamheshimu sana. Nilimkosea sana kwa sababu huwezi kumpigia mwanamke mwingine na kumtumia pesa wakati umekaa sebureni na mwanamke mwingine. Kwa sasa namtakia mema ila anisamehe yeye na familia yake.


“Monalisa anajiheshimu sana na ana heshima yake kwenye hili taifa, mimi nikimuona tu Monalisa hivi, aaah, kwa kweli nampenda. Ikitokea akasema turudiane, aisee moto utawaka, narudisha majeshi ila siwezi kusahau maisha tuliyoishi naye,” amesema Dudu Baya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad