Elon Musk Amlipua Eminen Kumsapoti Kamala Harris na Obama

Elon Musk Amlipua Eminen Kumsapoti Kamala Harris na Obama

Elon Musk Amlipua Eminen Kumsapoti Kamala Harris na Obama

Mkurugenzi Mtendaji wa Tesla, Elon Musk, amemshambulia rapa Eminem kwa kumuunga mkono Makamu wa Rais Kamala Harris na rais wa zamani Barack Obama. Tukio hili lilitokea Jumanne, Oktoba 22, baada ya taarifa kusambaa kuwa Eminem atamtambulisha Obama kwenye kampeni ya Harris iliyofanyika Detroit.


Kupitia X (zamani Twitter), Musk alijibu chapisho lililomkosoa Eminem kwa hatua hiyo kwa kusema: "Mshiriki mwingine wa sherehe za Diddy." Kauli hiyo inahusisha ukosoaji dhidi ya sherehe za Diddy, ambazo zimeibua utata kufuatia kukamatwa kwake kwa tuhuma za usafirishaji haramu wa binadamu na njama za uhalifu.


Majibu ya Elon Musk hayakushangaza wengi, ikizingatiwa kuwa amekuwa akimuunga mkono waziwazi Donald Trump, mpinzani wa Kamala Harris kwenye kampeni za Urais, ambapo Marekani inatarajia kupiga kura Novemba 5 na kumchagua mmoja wao kuwa Rais wa taifa hilo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad