Naibu Rais wa Kenya aliyeondolewa madarakani, Rigathi Gachagua amesema kikosi chake cha ulinzi kimeondolewa na hivyo lolote baya litakalomtokea Rais William Ruto atawajibika.
Gachagua, ambaye anapinga mashtaka dhidi yake akisema yamechochewa kisiasa, amesema kwamba usalama wake uko hatarini.
Rigathi Gachagua ameitwa kuhojiwa katika Ofisi za Upelelezi (DCI) ikiwa ni baada ya kutoa madai ya kuwepo kwa majaribio ya kuuawa aliyoyatoa wakati akitoka Hospitali ya Karen
Katika barua ya wito, DCI amesema “Tunaelewa unyeti wa tuhuma ulizotoa na tunakuhakikishia kuwa suala hili litashughulikiwa kwa uzito unaostahili. Taarifa yako ni sehemu muhimu ya uchunguzi wetu.”
Akizungumza Oktoba 20, 2024, Gachagua aliwatuhumu baadhi ya Maafisa wa Usalama kuwa walitaka kumuua kwa kumuwekea Sumu kwenye chakula nyumbani kwake, Agosti, 2024.