"Polisi Hatujashindwa Kudhibiti Uhalifu" Kamanda Muliro



Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es salaam, SACP Jumanne Muliro amesema Jeshi la polisi halifurahishwi na matukio mbalimbali ya upotevu wa watu yanayotokea kwenye jamii kwani jukumu kubwa ni kulinda raia wote na mali zao.

Hayo ameyasema leo Oktoba 05,2024 kwenye kongamano la Kitaifa Dhidi ya Matukio ya kupotea kwa Raia hapa nchini, yaliyoandaliwa na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS).

"Sisi Jeshi la polisi, msifikiri kwamba mtu anapokuwa haonekani au amepotea kwamba tunakuwa na raha au furaha, haiko hivyo. Maana jukumu letu sisi ni kuhakikisha kwamba jamii inakuwa na amani na usalama." Amesema Muliro.

Muliro ameitaka jamii kuheshimu mamlaka za ulinzi kwani mamlaka hizo zina weledi wa kutosha na zinafanya kazi zao kwa kuzingatia misingi ya sheria kwani wakifanya kazi hizo kwa mihemko wanaweza kufanya uchunguzi ambao si wa haki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad