Huyu Hapa Mbadala wa Mchezaji Mo Salah Liverpool

 

Huyu Hapa Mbadala wa Mchezaji Mo Salah Liverpool

Kwa mujibu wa Fichajes, Liverpool wana malengo ya kuimarisha safu yao ya ushambuliaji na wako tayari kuingia mfukoni kumsajili nyota wa klabu ya Eintracht Frankfurt ya Bundesliga, Omar Marmoush.


Arne Slot na uongozi wa Liverpool umekuwa ukifuatilia kwa ukaribu uchezaji wa Mmisri huyo na wanajiandaa kuweka mezani ofa ya pauni milioni 50 ili kumvuta Anfield.


Kwa mujibu wa mwandishi wa habari Tarek Metwally, Omar Marmoush ana uwezo wa kuwa bora zaidi kuliko Salah ambaye kandarasi yake itatamatika mwishoni mwa msimu huu na kuna mashaka kama ataongeza mkataba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad