Jeshi la Polisi Lamkamata Kijana Aliyejerui na Kutishia Bastola Wakitoka Club Masaki




Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linamshikilia Derick Derick Junior (36), Mkazi wa Salasala Kinondoni kwa tuhuma za Kujeruhi na kutishia kwa silaha tukio lilitokea tarehe 27.10.2024 saa 12.30 asubuhi maeneo ya Masaki '1245 night club' Kinondoni ambapo mtuhumiwa alimjeruhi Julian Bujuru kwa kumpiga na kitako cha bastola pia kumjeruhi sehemu ya jicho na pua.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2024 Kamanda wa jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Muliro J. Muliro amesema kuwa Kitendo hicho hakikubaliki na ni kinyume na sheria na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka linakamilisha utaratibu wa kisheria ili mtuhumiwa aweze kufikishwa katika Vyombo vingine vya Sheria haraka iwezekanavyo huku akiongeza kuwa kijana aliyejeruhiwa anaendelea vizuri na matibabu.

Jeshi la Polisi limetoa wito kwa wananchi kuwa halitasita kumchukulia hatau mtu yoyote anayemiliki silaha, atakayebainika kufanya matendo ambayo ni kinyume na Sheria Kanuni na taratibu zilizoainishwa katika kibali chake cha kumiliki silaha.

Habari zetu zinapatikana pia kwenye mtandao wa Onasasa,install app playstore au appstore kisha follow account yetu ya Middle simba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad