Joyce Ajiteka ili Amrudishe Mumewe Nyumbani

Joyce Ajiteka ili Amrudishe Mumewe Nyumbani


Joyce Ojala (32), Mkazi wa Matalawe Mjini Njombe, anashikiliwa na Polisi kwa kosa la kutoa taarifa za uongo kuwa ametekwa na Watu wasiojulikana ili kumlazimisha mumewe Mfaume Hussein Mzee (37), aliyekuwa Mkoani Ruvuma kwa zaidi ya miezi sita akifanya kazi za madini kurejea nyumbani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Mahamoud Banga, amethibitisha kuwa Joyce alitoa taarifa kwa Mume wake akidai ametekwa na kwamba Mume wake anatakiwa kurudi haraka ili kushughulikia suala hilo, Mfaume alipokea taarifa hizo na kuamua kurejea mara moja baada ya kuambiwa kuwa mkewe yuko hatarini lakini baada ya ufuatiliaji wa Polisi ilibainika kuwa hakuna tukio la utekaji na kwamba Mwanamke huyo alijiteka mwenyewe kutokana na wivu wa mapenzi.

Kamanda Banga ameendelea kueleza kuwa Mume huyo alikuwa akiwasiliana na Mke wake mara kwa mara na kumjulisha kuwa anafanya shughuli za madini na hana uwezo wa kurudi mara moja hata hivyo Mwanamke huyo aliingia wivu na kuamua kutengeneza kisa hicho cha utekaji ili kumfanya Mume wake kurudi, Polisi walifuatilia tukio hilo baada ya taarifa kupokelewa na mwishowe walimkuta Joyce akiwa amejificha katika kibanda cha Fundi seremala Mjini Njombe.

Mfaume alipofika nyumbani baada ya kurudi kutoka Ruvuma alikuta Nyumba yao imefungwa na akaamua kusubiri hadi asubuhi kabla ya kutoa taarifa kwa Polisi ndipo Polisi walipoanza ufuatiliaji wa tukio hilo na kugundua kuwa Joyce alikuwa amepeleka taarifa za uongo kwa lengo la kumrudisha Mume wake.


Joyce Ojala sasa anashikiliwa na Jeshi la Polisi huku hatua za kisheria zikichukuliwa kutokana na kosa hilo la kutoa taarifa za uongo. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad