Makamu wa Rais Nchini Marekani ambaye pia ni mgombea urais wa Chama Cha Democratic Kamala Harris ameahidi kuhalalisha bangi ndani ya taifa la Marekani, endapo atachaguliwa kuwa rais wa nchi hiyo kama sehemu ya mpango wake mkubwa wa "Opportunity Agenda.
Harris akiwa mstari wa mbele katika kuondoa sheria zilizopo zinazozuia matumizi ya bangi ambapo amesisitiza dhamira yake ya kubadilisha sheria za sasa.
"Hakuna hata mmoja anapawswa kwenda jela kwa kisa cha uvutaji Bangi," alisema Kamala Harris.
Dhamira yake kuu ni kuondoa vikwazo vya kisheria vinavyohusiana na bangi na kuleta mabadiliko ya haki kwa watu walioathirika na sheria za mwanzo.
Kauli hii imevutia mijadala kuhusu mabadiliko ya sera za bangi nchini Marekani, huku wengi wakisubiri kuona hatua zitakazochukuliwa ikiwa atashinda urais.