Kanisa Refu zaidi Duniani Lilijengwa Kwa Miaka 600
Kama siyo wewe basi wengi hamjasikia bado. Unaijua Cologne Cathedral? Hili ni moja kati ya makanisa makubwa na maarufu zaidi duniani. Lipo katika jiji la Cologne nchini Ujerumani.
Ujenzi wa kanisa hili ulianza rasmi mwaka 1248. Ilipofika 1473 ujenzi ulisimama, na hii ni kutokana na ukosefu wa fedha na teknolojia ya kukamilisha. Hata hivyo ujenzi uliendelea tena na kukamilika rasmi 1880. Zaidi ya miaka 600 baada ya kuanza.
Katika vita vya pili vya dunia, kanisa hilo lilinusurika vibaya na mashambulizi ya mabomu, na baada ya vita kuisha ukafanyika ukarabati mdogo ili kurudi kwenye hali yake.
Urefu wa kuta zake mbili zina urefu wa mita 157, na kuwa moja ya majengo marefu zaidi ya kanisa duniani. Hili ni kanisa la pili kwa ukubwa Ulaya. Eneo lake ni mita za mraba zaidi ya 7,000 na linahudumia zaidi ya watu 20,000 kwa wakati mmoja.
Mwaka 1996, Cologne Cathedral, liliorodheshwa kama sehemu ya urithi wa dunia na UNESCO. Hii ni kutokana na umuhimu wake wa kihistoria na usanifu wake wa pekee.
Kanisa hili lina kengere kubwa zaidi kuliko zote duniani. Kengere ya Peter (St. Peter's Bell) ina uzito wa zaidi ya tani 24. Yaani lori tatu za mchanga na zaidi.