Kanye West Ashitakiwa Kwa Unyanyasaji wa Kijinsia...


Lauren Pisciotta, aliyekuwa msaidizi wa Kanye West, amewasilisha kesi mpya akidai kuwa alileweshwa kwa madawa na kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia alipokuwa kwenye studio na bosi wake wa zamani pamoja na Sean "Diddy" Combs.

Kulingana na malalamiko hayo, Pisciotta anadai kuwa aliwekewa dawa kwenye kinywaji chake ambacho alipewa katika kikao hicho kilichofanyika studio huko Santa Monica. Kanye West, mwenye umri wa miaka 47, ndiye anayetuhumiwa kuagiza kinywaji hicho, ingawa Combs, 54, ambaye pia alihudhuria kikao hicho, hajatajwa kwa makosa yoyote.

Lauren Pisciotta anadai baada ya kunywa kinywaji hicho, alihisi kutojitambua vizuri na kushindwa kudhibiti mwili wake. Siku iliyofuata, alijikuta akiwa na hali mbaya na aibu kubwa, lakini hakuwa na ufahamu kamili wa kilichotokea. Anasema aligundua baadaye kwamba aliweza kufanyiwa unyanyasaji wa kijinsia baada ya Kanye West kukiri kuwa walikuwa "wamefanya kitu" usiku huo.

Madai haya ni sehemu ya kesi iliyowasilishwa Juni 2024 ambapo Lauren Pisciotta anamtuhumu Kanye West kwa unyanyasaji wa kijinsia na kuachishwa kazi kinyume n utaratibu. Wanasheria wa Ye wamekanusha madai hayo na kudai kuwa Pisciotta alikuwa anajaribu kumdharirisha Kanye baada ya kuachishwa kazi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad