Khalid Aucho: Mzize ni Fiston Mayele wa Baadae, Bado Mdogo




"Huwezi kumzuia mtu kutumia mitandao ya kijamii, atataka kupost kitu na ataona tu, hivyo huwezi kumzuia, ila ninachoweza kumuambia ni kuwa imara kiakili kwani kukosolewa kupo tu.

Hata Lionel Messi huwa anakosolewa, Ronaldo anakosolewa hata Neymar alikuwa anasemwa vibaya na mashabiki wake, au nchini kwao Brazil, ila haukati tamaa, unazidi kupambana mpaka ufikie lengo lako na Clement naamini atafika mbali zaidi.

Kwa sababu ana kila uwezo wa kufika mbali kwa kuwa nI mchezaji mzuri na atakuwa mzuri zaidi ya hapa alipo ana ''work rate" kubwa, bado mdogo, ana umaliziaji mzuri, spidi na nguvu.

Hivyo mashabiki kwa Tanzania, sio tu wa Yanga ila Taifa zima kwa kuwa kijana ni Mtanzania wanapaswa kumpa nguvu, kumshauri na kumsihi awe bora zaidi na sio kumtusi na kumkejeli na kwa sababu huyu ni Mtanzania na wanapaswa wampende maana ndio anakuja kuwa Samatta ajaye sasa kama tukimtusi sasa nani atakuja kumrithi Mbwana Samatta?

Kuna Musonda, Baleke na Dube ila unaona jinsi anapambana mpaka mwalimu anampa nafasi na ni mchezaji mzuri mkubwa ukizingatia anacheza nafasi moja na Musonda anayecheza timu ya Taifa ya Zambia na Dube anayecheza timu ya Taifa ya Zimbabwe na Baleke pia mchezaji mzuri, ina maana anafanya vizuri.

Hivyo inapaswa tu tumpe ushirikiano na nguvu, tusimuangushe" @auchokhalidofficial
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad