Iran imerusha makombora zaidi ya 200 kwenda Israeli katika kile kinachosemekana ni kulipa kisasi kutokana na kuuliwa kwa viongozi mbalimbali wa vikundi vya wanamgambo wanaoungwa mkono na Iran.
Shambulio la leo limefuatia vifo vya viongozi wa Hezbollah na Hamas, akiwemo Hassan Nasrallah aliyeuawa katika shambulizi la angani la Israel huko Beirut Septemba 27, 2024.
Makombora mengi yamedunguliwa na mfumo wa ulinzi wa Israel huku mengine yakifanikiwa kupenya bila kudunguliwa.
Mpaka sasa Israeli haijatoa tamko kuwa italipiza kisasi au la lakini imawaelekeza raia wake kujihifadhi katika vyumba vilivyoandaliwa maalumu kwa ajili ya kujilinda endapo kutatokea mashambulizi. Pamoja na kutozungumzia kisasi, Israeli huwa haikubali kutolipiza kisasi.
Iran imesema kuwa mashambulizi hayo ni hatua ya kwanza, ikionya kuwa mashambulizi zaidi yanaweza kufuata endapo Israel itajibu chochote.
Kwa upande wake, Marekani imeionya Iran kuhusu matokeo ya mashambulizi hayo, na imetangaza msaada wake wa kijeshi kwa Israel kupambana na tishio hilo.