Kipa Diarra, Dickson Job na Musonda Kuukosa Michezo wa Leo na Costal Union



Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe ameeleza kuwa golikipa wa timu hiyo Djigui Diarra ataukosa mchezo wa leo dhidi ya Coastal Union kwakuwa ana kadi tatu za njano.

Tutawakosa wachezaji kadhaa akiwemo Djigui Diarra ambae yupo nje kwasababu za kikanuni yeye amepata kadi tatu za njano hivyo ataukosa mchezo huu. Lakini pia tutamkosa Dickson Job na Kennedy Musonda ambao wana ‘injury’ na wengine kwasababu mbalimbali za kiufundi”
Amesema afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe.

Yanga wakiwa ugenini leo watakipiga dhidi ya Coastal Union majira ya saa 10:15 jioni katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad