Kocha Mwambusi Apewa Kazi Coastal Union.....Akaribishwa Kwa Mbwembwe


 Kocha Mwambusi Apewa Kazi Coastal Union.....Akaribishwa Kwa Mbwembwe

Klabu ya Coastal Union imemtangaza kocha Juma Mwambusi kuwa kocha mkuu klabuni hapo akichukua mikoba ya David Ouma aliyetupiwa virago.


“Ubora, weledi, mipango, mikakati na uwezo wako kila Mtanzania anaujua. Sasa malengo yetu ya kumaliza moja kati ya nafasi nne za juu yanakwenda kutimia 100%.” imesema taarifa ya Wagosi hao wa Kaya.


“Karibu sana mwalimu Juma Mwambusi, standard yako ni kufundisha klabu kubwa na kongwe hapa nchini. Wanamangushi Wanajua uwezo wako na spirit yako ya kupambania alama 3 kwa kila mchezo.”


“Karibu baba,karibu master,karibu ‘silent killer, karibu mkuu wa benchi la ufundi na kocha mkuu Juma Mwambusi.” —— Coastal Union

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad