Kutana na Aghoris Jamii ya Kihindi Wanaokula Nyama za Binadamu Aliyefariki...


Aghoris ni kundi la Wahindi ambao huchagua kuishi kwa hiari kwenye mahali pa kuchomea maiti, na baada ya maiti kuchomwa moto, huvuta moshi wa maiti, hutumia majivu yaliyobaki kama mapambo kwenye miili yao, hula nyama ya binadamu aliyekufa na kunywa haja ndogo zao wenyewe. Hutumia mifupa ya waliofariki kuunda vitu mbalimbali pia hutumia mafuvu ya binadamu kama mabakuli ya chakula.

Kundi hili la Aghoris huwa haliui watu ili kutafuta nyama za kula bali wanasubiri wale ambao tayari wamefariki.

Kundi hili linaamini kwamba kifo ni kitu cha kawaida sana na kila mtu lazima apitie hatua hiyo pia wanaamini kwamba binadamu lazima aishi kulingana na mazingira.

Jamii hii inakadiriwa kuwa ina jumla ya watu 82,000, wanapatikana kwa wingi Veranasi, India Kusini.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad