Kwani Kuna Tatizo kwa Mwanamke Kumtongoza Mwanaume?

 

Kwani Kuna Tatizo kwa Mwanamke Kumtongoza Mwanaume?

Daunia inakwenda kwa kasi kwelikweli, yale ambayo miaka kadhaa iliyopita yalikuwa hayawezekani, hivi sasa yanawezekana.


Utandawazi umeleta mabadiliko makubwa katika maisha ya kila siku na mambo mengi yamebadilika kabisa. Miaka ya nyuma, ili mwanaume na mwanamke waanzishe uhusiano ambao baadaye utakuja kuzaa uchumba na hatimaye ndoa, ilikuwa ni lazima mwanaume ‘amfukuzie’ kwelikweli mwanamke anayempenda! likuwa siyo ajabu kabisa kwa mwanamke kumzungusha mwanaume miezi kadhaa kabla ya kumpa majibu. Lakini hivi sasa mambo yamebadilika, njia za kuanzisha uhusiano mpya zimekuwa nyingi kiasi kwamba hata muda wa ‘kufukuziana’ umepungua sana.


Si ajabu tena kuona watu wamekutana leo, kesho wakaingia kwenye uhusiano na miezi kadhaa baadaye wakaoana au wakavurugana na kushindwa kutimiza malengo ya kuingia katika ndoa. Yote kwa yote, maisha yanazidi kusonga mbele. Hivi umewahi kujiuliza, kuna tatizo gani kwa mwanamke kumtongoza mwanaume? Ni kweli kwamba ukiona mwanamke amepata ujasiri wa kumwambia mwanaume kwamba anampenda, basi huyo ana tabia mbaya, hajatulia na hafai kuingia naye kwenye uhusiano wa kimapenzi?


Ni kweli kwamba mwanamke anatakiwa kusubiri kutongozwa tu, hata kama yupo mtu anayempenda; hana uhuru wa kumweleza kwa sababu mila na desturi za Kitanzania haziruhusu? Hebu tushirikishane mawazo hapa, kuna tatizo gani kwa mwanamke kumtongoza mwanaume? Nimekuja na mada hii baada ya kuzungumza na mmoja kati ya wasomaji wangu, ambaye yeye ni mwanamke aliyefikia umri wa kuolewa lakini kuna kitu kinamsumbua sana.


Amenieleza kwamba kwa mara ya mwisho, alikuwa kwenye uhusiano karibu mwaka mmoja uliopita lakini yalitokea matatizo kati yake na huyo mpenzi wake, yaliyosababisha uhusiano wao uvunjike kabla ya kufikia hatua ya kuingia kwenye ndoa.


“Kuanzia kipindi hicho, nimekuwa nawachukia sana wanaume, nawaona kama wote ni walewale na hata mtu akinitongoza nakuwa mkali kwelikweli. Lakini katika siku za hivi karibuni, kuna kaka mmoja mgeni amekuja kazini kwetu, naye ameajiriwa kama sisi. “Kiukweli nikimtazama huyu kaka moyo wangu unafurahi sana, namuona yupo tofauti na wanaume wengine, kwanza ni mpole, ana heshima, ana busara na pia mwonekano wake unaniridhisha na bado hajaingia kwenye ndoa kama mimi.


“Najaribu kumuonesha kwa vitendo kwamba nampenda lakini naona kama hanielewi, natamani kumtamkia ili anielewe lakini naogopa jamii inaweza kunitafsiri vibaya, nimebaki na mateso tu ndani ya moyo wangu. Tafadhali nisaidie nifanye nini ili kumfikishia ujumbe huyu kaka?” Hayo ni maelezo ya huyu dada yetu kama nilivyomnukuu na kwa sababu ya tatizo linalomsumbua, ndiyo nikaamua kuja na mada hii kama inavyojieleza hapo juu.


Je, kuna tatizo lolote kama huyu dada atamfuata mhusika na kumweleza wazi kwamba anampenda?


Uhusiano ambao mwanamke ndiye aliyemtongoza mwanaume, unaweza kuwa imara na kufikia hatua ya ndoa?

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad