MAJINA YA WASHIRIKI WA P DIDDY KUTAJWA, UNAAMBIWA DUNIA ITASIMAMA KWA MUDA

MAJINA YA WASHIRIKI WA P DIDDY KUTAJWA, UNAAMBIWA DUNIA ITASIMAMA KWA MUDA

Orodha ya wanaodaiwa kuwa Washirika wa Msanii wa Marekani, Diddy Combs anayetuhumiwa kwa makosa ya unyanyasaji, ulaghai na biashara ya ngono inatazamiwa kutajwa hivi karibuni katika hatua nyingine ya kesi zinazomkabili, Wakili mtetezi wa Waathirika wa matukio hayo Tony Buzbee amethibitisha.

Buzbee ameviambia vyombo vya Habari kuwa “majina hayo yatawashtua.” wakati akitangaza kesi mpya zilizofunguliwa dhidi ya Msanii huyo kwa niaba ya Waathiriwa 120 wanaodai kunyanyaswa kingono na Diddy, amesema “siku itakuja ambapo tutataja majina mengine isipokuwa Sean Combs, na kuna majina mengi.” amedokeza.

Wakili huyo ameongeza kuwa kwa sasa ana mpango wa kuwasilisha kesi hizo katika majimbo kadhaa kwa muda wa siku 30 zijazo na ameahidi kufichua majina hayo baadaye pia amethibitisha kuwa nusu ya Walalamikaji ni Wanaume na kwamba mashambulizi mengi yanayodaiwa yalifanyika New York, California, Georgia na Florida.

Malalamiko 120 ambayo ametangaza kwa sasa yanaanzia katika kesi za mwaka 1991 huku Mshukiwa mdogo kabisa anayedaiwa kunyanyaswa na Msanii huyo ametajwa kuwa Mtoto wa umri wa miaka tisa tu huku wanaomshtaki Diddy wengine 25 wakisema kuwa walikuwa Watoto wadogo wakati Msanii huyo anawatendea uhalifu huo.

Haya yote yanakuja baada ya Diddy mwenye umri wa miaka 54 kufunguliwa Mashtaka katika Mahakama ya Shirikisho Nchini Marekani kwa makosa ya ulaghai na biashara ya ngono, hata hivyo Msanii huyo amekanusha makosa yote na amekana hatia ya madai ya jinai huku akiendelea kushikiliwa katika gereza la Metropolitan bila dhamana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad