Makubwa...Dereva wa Basi la Abiria Akutwa na Leseni ya Pikipiki

 

Makubwa...Dereva wa Basi la Abiria Akutwa na Leseni ya Pikipiki

Jeshi la polisi linamshikiria dereva wa basi lenye namba za usajili T622 EFG linalofanya safari zake kutoka jijini Mwanza kwenda Morogoro kwa kosa la kukutwa na leseni ya pikipiki ili hali akiwa ni dereva wa gari la abiria.


Hayo yamebainishwa na kamanda wa kikosi cha usalama barabarani DCP. Ramadhan Ng’anzi leo Oktoba 25, 2024 wakati wa operesheni ya ukaguzi wa magari yanayobeba abiria yanayofanya safari za usiku kutoka jijini Mwanza kuelekea mikoa mingine iliyofanyika katika eneo la Tinde mkoani Shinyanga


Akizungumza mara baada ya zoezi hilo DCP. Ng’anzi amesema katika ukaguzi huo walioufanya takribani magari 53 yamekaguliwa ambapo magari 15 yamekutwa na makosa mbalimbali huku magari 2 yakizuiliwa kutoendelea na safari kutokana na ubovu wa magari hayo.


Aidha DCP. Ng’anzi amebainisha kuwa mpaka sasa madereva 105 hapa nchini wamekwisha fungiwa leseni zao kwa kushindwa kufuata sheria za usalama barabarani kwa muda usiopungua miezi 6.


Nao baadhi ya abiria wamelishukuru jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani kwa kuendesha oparesheni hiyo jambo litakaloweza kubaini makosa mbalimbali na kupunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na uzembe wa madereva na ubovu wa magari.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad