MAKUBWA...Mtoto wa R Kelly Afunguka Baba yake Huyo Kumnyanyasa Kingono Akiwa Mtoto

MAKUBWA...Mtoto wa R Kelly Afunguka Baba yake Huyo Kumnyanyasa Kingono Akiwa Mtoto


Binti wa R. Kelly, Buku Abi, amezungumza hadharani kwa mara ya kwanza kuhusu madai ya unyanyasaji aliofanyiwa utotoni na baba yake, akielezea hofu yake ya kumwambia mtu wakati huo.


Kupitia filamu mpya *R. Kelly Karma: A Daughter's Journey*, iliyozinduliwa leo, Abi mwenye umri wa miaka 26, alifunguka kwa hisia, akisema kwamba alidhulumiwa na mwimbaji huyo akiwa mtoto. Alisema aliripoti kwa mama yake, Andrea, tukio hilo mwaka 2009, wakati alipokuwa na miaka 10.


"Alikuwa kila kitu kwangu. Kwa muda mrefu, sikutaka hata kuamini kwamba ilitokea. Sikujua kuwa, hata kama angekuwa mtu mbaya, angeweza kunifanyia kitu kama hiki," alisema Abi kwa huzuni.


"Niliogopa sana kumwambia mtu yeyote; niliogopa kumwambia mama yangu," aliongeza.


Kwa mujibu wa *The People*, Abi alisema baada ya tukio hilo aliogopa kuzungumza hadharani, lakini aliamua kumpa mama yake taarifa hizo na kusitisha kwenda kumuona baba yake wakati huo.


Kumbuka kwamba R. Kelly kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 20 jela kwa kosa la unyanyasaji wa kingono kwa watoto wa chini ya umri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad