Mama Yake P Diddy Afunguka ya Mwanaye "Wanamwonea Mwanangu"

Mama Yake P Diddy Afunguka ya Mwanaye "Wanamwonea Mwanangu"


Mama yake Sean "Diddy" Combs, Janice Smalls Combs, amejitokeza kumtetea mwanawe wakati anakabiliwa na kesi za biashara ya binadamu kwa ajili ya ngono na tuhuma nyingi za unyanyasaji wa kijinsia.

Kwenye taarifa aliyoitoa kupitia wakili wake kwa #PageSix Janice alisema inavunja moyo kuona mwanae akihukumiwa kwa "stori iliyotengenezwa kwa uongo" badala ya ukweli.

Janice alikiri kuwa Diddy si mkamilifu na amefanya makosa, akielezea kuwa alikosea kwa kutokubali ukweli kuhusu vurugu dhidi ya mpenzi wake wa zamani, Cassie, kama ilivyoonyeshwa kwenye video za hotelini.

Pia alielezea kuwa uamuzi wa Diddy kumaliza kesi ya Cassie nje ya mahakama ulitokana na hofu ya ukweli kuwa tata na ngumu kueleweka.

Janice aliendelea kusema kuwa, kutoeleza ukweli kwa uwazi kwenye suala moja hakumaanishi Diddy ana hatia ya madai mazito yanayomkabili. Alitoa mfano wa watu walionyimwa haki zao kutokana na historia yao ya zamani, akisisitiza kuwa kila mtu anastahili kusikilizwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad