Maskini Mtiga Abdallah Aliyekuwa Mtangazaji wa The Story Book Afunguka Jinsi Diamond Anavyomdhibia Riziki

 

Maskini Mtiga Abdallah wa The Story Book Aamua Kufunguka Jinsi Maneno ya Diamond Yanavyomkosesha Ridhiki

Baada ya Mtiga Abdallah kuondoka Wasafi Media kisha Jamal April akaanza kutangaza The Story Book, Diamond Platnumz alimkaribisha Jamal kwa kuandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa Jamal pia asifanye "The Story Book" mbili au tatu kisha akisifiwa kidogo tu aanze kuvuta bangi, kunywa pombe, kuchelewa kazini, kujikuta mwamba au kuvimba kuwa hakuna The Story Book bila yeye.


Maneno hayo yalifanya watu wengi waamini kuwa huenda Mtiga alifukuzwa Wasafi Media kutokana na tabia hizo ambazo Diamond Platnumz hataki Jamal April awe nazo.


Kwa muda wote tangu Mtiga aondoke alikuwa kimya sana ila leo kwenye "Birthday" ya Diamond Platnumz ameamua aanike yote na kueleza kuwa kauli hiyo mpaka leo inamkosesha fursa mbalimbali maana wengi wanaamini meneno hayo.


"Happy BirthDay Boss Diamond Platnumz, Sheikh Mansour Naomba nitumie siku yako ya kuzaliwa kukuambia Kuwa Maneno uliyowahi kuyasema Mwaka 2020 yamekuwa yakinirudisha Sana nyuma na kunifungia milango.


Kila mlango ninaojaribu kuufungua inashindikana taswira uliyonijengea imekuwa ni kikwazo kikubwa Sana kwenye maisha yangu ya utangazaji ukizingatia bado ni kijana na nyuma yangu Kuna watu wengi wananitegemea.


Binafsi ninaelewa kwanini ulifanya vile na ndiyo maana sikujitokeza kujibu Wala kujitetea hata pale Online Medias waliponitafuta. Ninajua Kuwa nilitumika kama Daraja ili mwenzangu apate nafasi, lakini ukweli ni Kuwa wewe ni msanii mkubwa na utafatiliwa na watu wengi sana so neno lako bila ya kutarajia linaweza kumuathiritu mwingine.


Uliongea maneno ya uongo ili tu watu wampokee Jamal najua ulifanya makusudi cz nilikuwa najua Kila kitu kinachoendelea lakini watu wa nje hawajui Hilo wanaamini maneno yako na yametumika Sana kunizibia njia yangu ya ridhki," amesema Mtiga Abdallah

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad