Maskini Mutale, Wachambuzi wa Michezo Waanza Kumsulubisha Wadai Kiwango Hana

Maskini Mutale, Wachambuzi wa Michezo Waanza Kumsulubisha Wadai Kiwango Hana


Ameandika Mchambuzi Kelin Robson:

Joshua Mutale Budo Mutale sio yule aliyekuwa Power Dyanamos msimu uliopita …. Mwamba alikuwa hatari sana (Kasi , maamuzi sahihi + utengenezaji, kiukweli performance yake imeshuka sana tangia ajiunge na Simba : hana utulivu , umakini , poor decision anapoteza mipira kirahisi sana .

Fadlu Davids anazidi kumpa nafasi Budo Mutale lakini mwamba bado aoneshi mabadiliko ya ubora wake : Nafikiri yupo hatarini sana kupoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza .

Hans Rafael Ameandika:

Mutale ana kipaji kikubwa sana,ana kasi na ujuzi wa kuwatoka walinzi ila kusema ukweli mazingira ya Bongo bado hayajamkubali.

Muda mwingi anapoteza mipira,lakini pia anachelewa kwenye baadhi ya matukio muhimu.

Pressure ya Simba na Yanga ni kubwa sana…anatakiwa kujiangalia.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad