Mchezaji Aomba Radhi kwa Kuwarekodi Wanawake Video za ngono bila ridhaa yao

 

mchezaji Aomba Radhi kwa Kuwarekodi Wanawake Video za ngono bila ridhaa yao

Mshambuliaji wa soka wa Korea Kusini Hwang Ui-jo ameomba radhi kwa kuwarekodi Wanawake filamu za ngono bila ridhaa yao.


Waendesha mashtaka wameeleza kuwa kati ya mwezi Juni na Septemba 2022, Hwang (31) alirekodi video hizo kwa siri, mara nne tofauti.


Video hizo zilipostiwa katika mitandao ya kijamii na shemeji wa mchezaji huyo ili kumsaliti.


Hwang alimfungulia kesi mwanamke huyo, ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela.


Akizungumza katika Mahakama jijini Seoul, Hwang amesema “ninaomba msamaha sana kwa huzuni niliyosababisha, sitarudia tena, kuanzia sasa nitapambana kuwa Mwanasoka mwema”


“Naomba radhi kwa waathirika wa suala hili, na wengine wote wanaonijali ambao nimewasikitisha”.


Mwezi uliopita mshambuliaji huyo wa zamani alihama kutoka timu ya Nottingham forest ya Uingereza na kuhamia Alanyaspor ya Uturuki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad