Hapo awali uongozi wa Yanga ulifanya kila linalowezekana ili kuipata saini ya mchezaji huyo hadi Rais wa Yanga alisafiri kwenda hadi Nchini DR Congo akakutana na Rais wa timu ya TP Mazembe Moise Katumbi kujadili uhamisho wa mchezaji huyo jambo ambalo lilishindikana kwakuwa mchezaji huyo alikataa kujiunga na Yanga kutokana na offer kubwa iliyokuja mezani kutoka kwa Raja Cassablanca kisha Rais wa yanga akaambulia kupiga tu picha na Rais wa Tp Mazembe na kisha kurejea nchini.
Mara baada ya dili la kutua Raja Cassablanca kuleta gagaziko basi mchezaji huyo alitua rasmi Club Africaine ambapo yupo hadi hivi sasa, mara baada ya Timu hiyo yake ya sasa kuridhia kuondoka kwa mshambuliaji huyo hatari kwenye eneo la winga basi uongozi unaomsimamia mchezaji huyo umefanya jitihada za kutimiza ndoto za kujiunga na msibazi na kila kitu kimekwenda vizuri kinachosubiriwa ni muda tu kijana kutua rasmi ndani ya mitaa ya msimbazi na uhuru kariakoo