Katika hali isiyo ya kawaida mchezaji wa timu ya Taifa ya Zambia Evans Kangwa ameondoka kwenye kambi ya timu yake ya Taifa wakati wakijiandaa kusafiri kuelekea Ypunde Cameroon kwa ajili ya mechi ya marudiano dhidi ya Chad katika kampeni ya kufuzu AFCON 2025,
Mshambuliaji huyo ambaye anakipiga katika timu ya ligi kuu ya China amewaaga wachezaji wenzake na kuwaambia haoni sababu ya kuendelea kuwepo kambini ni sawa na kupotez muda ni bora akaipambanie klabu yake huko China,
Kangwa amewaambia viongozi wa chama cha soka nchini humo kwamba amechagua kutoenda Cameroon kwa sababu mbali mbali ikiwemo umuhimu wake kwenye klabu yake,
Taarifa kutoka kwa watu wa karibu wa mshambuliaji huyo ni kwamba amechukizwa na kitendo cha kocha Avram Grant kumuweka benchi katika mechi ya nyumbani dhidi ya Chad ambapo mshambuliaji Kennedy Musonda alicheza kwa dakika zote 90
Zambia itakabiliana vikali dhidi ya Chad jumanne hii ugenini huko Cameroon katika kuwania nafasi ya kufuzu AFCON nchini Morocco
Ikumbukwe kuwa tayari Zambia imethibitisha kukosekana kwa kiungo Clatous Chota Chama kabla ya Jumanne.