Mke wa Mume Aliyeuawa na Wadai MIKOPO Afunguka "Nilikopa Bila Kumwambia Mume"

Mke wa Mume Aliyeuawa na Wadai Mikopo Afunguka "Nilikopa Bila Kumwambia Mume"


Mke wa Mfanyabiasha na Mkazi wa Mbagala Mlandizi Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, Juma Said Mfaume (40) aitwaye Khadoja Ramadhanni amewaomba Walimwengu wamsamehe akisema anajiona Mkosaji kwa kukopa Tsh. laki 3 bila kumshirikisha Mumewe na mwisho kupelekea kifo cha Mumewe baada ya kudaiwa kupigwa na Wafanyakazi wa kampuni aliyokopa ambao walifika nyumbani kudai marejesho.

Mke wa marehemu Khadija amesema “Nilikopa Tsh laki 3 ya kwanza kwa kushirikiana na Mume wangu tukarudisha marejesho yakabaki matatu, wakaja wakaniambia umekaa muda mrefu muda umepita itabidi tukupe hela umalize deni ili tuanze upya, nikawaambia Mume wangu alisema nisichukue wakaanza kunijazia Watu nikakubali mkopo mpya na kuanza kurejesha kimyakimya bila kumwambia Mume wangu, baadaye walimfuata Mume wangu akauliza nikamwambia nimelipa deni na nyingine nimenunua smartphone nikamuomba msamaha”

“Mume wangu akanielewa akasema nitakusaidia kulipa Tsh laki 1 kwenye deni , rejesho kila Wiki ni Tsh. elfu 34 lakini nashangaa naambiwa wamekuja wamemshambulia na kumuua walisema wanataka dhamana Mume wangu akabisha maana sio yeye aliyenidhamini, namuomba Rais Samia Mwanamke mwenzangu anisaidie sheria ifuate mkondo wake waadhibiwe, maana Mimi ndiye mwenye makosa nimemponza Kijana wa Watu amepoteza maisha, nisameheni Walimwengu”

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani limethibitisha kuwashikilia Wafanyakazi wanne wa kampuni ya utoaji mikopo kwa tuhuma za mauaji ya Juma Said Mfaume (40), ambapo walifika nyumbani kwa Marehemu kwa lengo la kudai fedha za marejesho ya mkopo kwa Mkewe na baada Juma kuwaeleza kuwa mkewe hayupo walilazimisha kuingia ndani kwa nguvu ili wachukue vitu kama dhamana huku wakimshambulia sehemu mbalimbali za mwili wake kwa kutumia fimbo na baadaye alianguka chini na kupoteza fahamu na baadaye akafariki Dunia.

Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani, Muhudhwari R. Msuya - ACP amesema baada ya Watuhumiwa hao kuona Juma amepoteza fahamu walimbeba kwa kutumia gari lao ili wampeleke Kituo cha Afya Mlandizi na alifariki akiwa anapatiwa matibabu Kituoni hao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad