Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Camillus Wambura


MKUU wa Kituo cha Polisi Wilaya ya Makete, mkoani Njombe, anadaiwa kumkamata mwananchi, Levis Mahenge, kumpeleka Kituo cha Polisi na kumpiga hadi kumvunja mkono.


Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi nchini kupitia Msemaji wake, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) David Misime, katika taarifa yake jana, alieleza hatua ambazo zimeshachukuliwa dhidi ya kiongozi huyo.


“Ufafanuzi ni kwamba, tukio hilo lilitokea Oktoba 9, mwaka huu, saa 12:30 jioni. Baada ya tukio hili kugundulika na uongozi wa Polisi Mkoa wa Njombe, jalada lilifunguliwa na ushahidi ukakusanywa na uchunguzi umekamilika.


“Hivi sasa hatua za kinidhamu zinaendelea kukamilishwa dhidi ya mkuu wa kituo hicho na baada ya hatua hizo, kwa sababu tuhuma zinazomkabili ni za kijinai zitafuata,” alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad