MUNA Love Achafukwa na Emmanuel Mbasha Kutangaza Amezaa Naye "Sitaki Drama"

MUNA Love Achafukwa na Emmanuel Mbasha Kutangaza Amezaa Naye "Sitaki Drama"


Munalove, kupitia ukurasa wake wa Instagram, amemkemea vikali Emmanuel Mbasha kwa kile alichokitaja kama kueneza uongo na kutumia mtoto wake kwa kiki za mitandaoni. Kwenye ujumbe wake, @munalove100 amesisitiza kuwa yeye na Mbasha hawajawahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi, na zaidi walikuwa marafiki kipindi cha nyuma. Munalove amesema kuwa Mbasha ameendelea kudai kuwa yeye ni baba wa mtoto wake, madai ambayo Munalove ameyakanusha waziwazi.

Munalove, ambaye alipoteza mtoto wake wa kwanza, Patrick, mwaka 2017, ameelezea huzuni yake juu ya jinsi Mbasha anavyotumia madai hayo ya uongo kuharibu jina la mtoto wake na kumtengenezea mazingira mabaya ya baadaye. Akiwa amechoshwa na hali hiyo, Munalove amemtahadharisha Mbasha kuwa ameweka mipaka na ameahidi kuchukua hatua zaidi endapo Mbasha ataendelea na vitendo hivyo vya kiki za kijinga.

Amesema, "Mbasha ifike mahali tuheshimiane, staki drama. Naomba uheshimu watoto na familia yako na kuacha kutumia jina la mtoto wangu kwa manufaa yako."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad