Mwanaume aitwae David McCulloch (41), aliyemfumania Mke wake akichepuka na Kaka yake (Jamie McCulloch) nyuma ya gari huku Mama yao (Mama wa Mwanaume) akiwa amekaa katika kiti cha Dereva, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela kutokana na kufanya fujo na kuwatishia kuwaua.
David amehukumiwa katika Mahakama Kuu ya Burnie iliyopo kaskazini mwa Jimbo la Tasmania huko Australia baada pia ya kukiri mashtaka ya udhalilishaji, kumiliki dawa za kulevya na bunduki ambapo kwa mujibu wa nyaraka za Mahakama, David aliwafumania wakifanya mapenzi nyuma ya gari kwenye maegesho ya magari yaliyopo karibu na anapoishi Jamie.
Tukio hilo ambalo lilimshangaza David hasa baada ya kumuona Mama yake amekaa bila wasiwasi, lilimpa hasira na kuanza kuwashambulia kwa kuwapiga Jamies na Mkewe na kupelekea majeraha ambayo yaliwafanya walazwe Hospitali.
Pamoja na kwamba David amehukumiwa kwenda jela, Hakimu alikiri Mahakamani kwamba sakata hilo lazima lilikuwaa la kukasirisha kwa David na kusema huo ni ukiukwaji wa uaminifu ndani ya Familia.
Wanandoa hao wamekuwa Wapenzi kwa miaka 25 na wana Watoto wanne ambapo waliamua kufunga ndoa miaka sita iliyopita na kuanza kuishi nyumba moja na Mama wa David aitwae Sue McCulloch.