Mwanamuziki Phina Aucheka Ushindi wa Zuchu Tuzo za TMA

Mwanamuziki Phina Aucheka Ushindi wa Zuchu Tuzo za TMA

Mwanamuziki Phina Aucheka Ushindi wa Zuchu Tuzo za TMA

Usiku wa Tuzo za Muziki Tanzania (@tanzaniamusicaward), mwanamuziki Phina alizua mjadala mzito kwenye mtandao wa instagram baada ya kupost picha iliyokuwa na emoji tano za kucheka. Tukio hili lilikuja mara tu baada ya kuikosa 'Tuzo ya Mtumbuizaji Bora wa Kike', ambayo iliondoka na Zuchu. Hali hii iliwafanya mashabiki wake na wapenzi wa muziki kutoa maoni yao mbalimbali, wengi wakihisi kuwa @phina__tz alikuwa akiwakejeli waandaaji wa tuzo hizo au hata Zuchu mwenyewe.

Baadhi ya mashabiki wa Phina walimpa moyo, wakisisitiza kuwa yeye ndiye anayestahili tuzo hiyo kwa uwezo wake mkubwa wa kutumbuiza. Moja ya mashabiki aliandika, "Sisi tunajua wewe ndo mtumbuizaji bora wa kike." Hawa waliona kuwa ingawa hakupata tuzo, Phina bado ni bora kwenye kazi ya utumbuizaji wa muziki wake.

Hata hivyo, mashabiki wa @officialzuchu walijitokeza kwa nguvu, wakimtetea msanii wao na kusema kuwa alistahili kabisa ushindi huo. Mmoja wao aliandika, "Zuchu amestahili tuzo zote, nyie wengine bebeni mimba!" Wakati huo huo, walimshauri Phina kuonyesha heshima kwa mshindi badala ya kufanyia mzaha tukio hilo.

Pamoja na hayo, kulikuwa na maoni ya kuchekesha ambapo baadhi ya watu waliona tukio hili kama sehemu ya burudani. Mmoja aliandika, "Miuno yote unayomwaga wamekunyima tuzo, cheka tu mama!". Huku wengine wakienda mbali zaidi na kuhusisha tukio la tuzo za muziki na masuala ya kisiasa.

Mjadala huu umeonyesha wazi kwamba muziki wa Tanzania una nafasi kubwa kwa mashabiki, na tuzo kama hizi zinaweza kuleta mijadala mikali, hisia kali, na hata utani wa hali ya juu.

Kwa ujumla, hisia zimegawanyika, huku wengine wakiona Phina alistahili zaidi, na wengine wakisimama na Zuchu kama mshindi wa haki.

✍️: @enkyfrank

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad