Mwanaume Mwingine Anaswa na Bunduki Kwenye Mkutano wa Donald Trump

 

Mwanaume Mwingine Anaswa na Bunduki Kwenye Mkutano wa Donald Trump

Mwanaume mwingine amekamatwa akiwa na bunduki, vifaa vya uandishi wa Habari vya uongo na tiketi za meza kuu akijaribu kuingia katika mkutano wa Kampeni za Donald Trump huko California, Marekani, Polisi wamethibitisha.


Mwanaume huyo ametambuliwa kama Vem Miller, ni Mkazi wa Las Vegas, rekodi za Polisi zinaonyesha kuwa alikua amefungiwa kutumia bunduki na kuachiliwa baada ya kuwekewa dhamana ya dola 5,000 (Tsh. milioni 13,607,470/-)


Huduma ya Siri ya Marekani imetoa taarifa ikisema kuwa iliarifiwa kuhusu kukamatwa kwa Mtu huyo na kwamba tukio hilo halikuathiri shughuli za ulinzi na kutoa shukurani zake kwa Maafisa wa Polisi waliosaidia kulinda usalama katika mkutano huo wa Trump.


Miller baadaye aliviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba alikuwa Mfuasi wa Trump ambaye alinunua bunduki hizo kwa usalama wake na kuwajulisha Polisi katika kituo cha ukaguzi kuwa zilikua kwenye gari lake “mashtaka haya ni ujinga kabisa, mimi siwezi kusababisha vurugu” amesema.


Ulinzi wa Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump uliimarishwa katika wiki kadhaa zilizopita baada ya Mamlaka za Marekani kudokeza kuwa Nchi ya Iran imepanga njama za kumuua Kiongozi huyo kutokana na kuamuru shambulio la ndege zisizo na rubani kumuua aliyekua Kiongozi wa Taifa hilo Qassem Soleimani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad