Naibu Rais mpya Kuapishwa Kenya Kesho, Mapumziko Nchi Mzima....




Serikali ya Kenya imetangaza kuwa kesho Ijumaa November 01,2024 ni siku ya mapumziko (Sikukuu ya Kitaifa) ambapo Wakenya hawatoenda makazini ili kupisha hafla ya kumuapisha Naibu Rais mpya wa Nchi hiyo Kithure Kindiki ambaye anachukua nafasi ya Righathi Gachagua ambaye ameondolewa madarakani na Bunge la Nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa leo October 31,2024 na Waziri Mkuu wa Baraza la Mawaziri, Musalia Mudavadi ambaye ameteuliwa na Rais Rutto kukaimu nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ambayo ilikuwa inashikiliwa na Kindiki, imesema kwamba kesho ni mapumziko hii ikiwa ni muda mfupi baada ya gazeti rasmi la Serikali kutangaza taarifa hiyo pia.

Uamuzi wa Kindiki kuapishwa umekuja muda mfupi baada ya Mahakama Kuu Nchini humo kuondoa amri iliyokuwa inamzuia kuapishwa .

Kindiki aliteuliwa na Ruto October 18, 2024, na kupitia kipengele cha 149 (1) cha katiba, Bunge la Kitaifa lilimuidhinisha Kindiki kuwa Naibu Rais Mteule lakini hata hivyo upande wa Naibu Rais aliyeondolewa madarakani uliwasilisha ombi la kuzuia kuapishwa kwa Kindiki Kithure kama Naibu Rais mpya, siku moja baada ya Bunge la Seneti kupiga kura ya kumuondoa Rigathi Gachagua madarakani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad