NINI KINAFUATA KWA AFANDE ALIEWATUMA NYUNDO NA WANZAKE? WAZIRI GWAJIMA AFUNGUKA

 

NINI KINAFUATA KWA AFANDE ALIEWATUMA NYUNDO NA WANZAKE? WAZIRI GWAJIMA AFUNGUKA

Nini kinafuata kwa "Afande" aliewatuma nyundo na wenzake? Waziri Gwajima aeleza

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na wenye Mahitaji Maalum, Dk Dorothy Gwajima, amezungumzia kifungo cha vijana wanne, maarufu ‘waliotumwa na afande’ kumbaka na kumlawiti binti wa Yombo Dovya.


Hii ni baada ya Waziri Gwajima kuposti katika mtandao wake wa X zamani Twitter, hukumu ya watu hao wanne ambao jana Septemba 30, 2024 walihukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa hilo, na baadaye wasomaji kumuuliza maswali.


Waliohukumiwa kifungo hicho na Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma ni askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), MT 140195 Clinton Damas, maarufu Nyundo, Amin Lema, Nickson Jackson na askari magereza C1693 Praygod Mushi.


Mmoja wa wasomaji hao aliandika “Tunashukuru kwa wote tuliochukizwa na lile tukio walau mmetufuta machozi. Watanzania hii ndio haki tunayoililia. Sasa swali vipi kuhusu afande?” aliuliza swali hilo kisha Waziri Gwajima akalazimika kumjibu.


“Najaribu kuwaza kama wewe kuwa hawa waliosema wametumwa wao si ndiyo wangethibitisha huko mahakamani ambako mimi na wewe hatukuwepo? Kumbuka mimi na wewe hatuna mamlaka ya kuingilia shauri la mahakamani...”


“Ila wao hao wahukumiwa ndiyo walikuwa na fursa ya kusema tulitumwa na fulani na ushahidi huu hapa na Mahakama iamue. Hivyo naomba niishie hapa kuheshimu maamuzi ya Mahakama kama tulivyosikia na ambaye hajaridhika nadhani huwa kuna fursa ya rufaa. Ahsante Sana,”alisema Waziri Gwajima.


Baada ya jibu hilo, mchangiaji mwingine akaandika “Afande ni muhimu”, na hapo Waziri Gwajima akajibu “Hao wahukumiwa sasa ndiyo wakate rufaa waihakikishie Mahakama kuhusu kutumwa kwao. Mimi na wewe wasikilizaji tuna wapokea matokeo maana wakati wakitumwa, sisi hatukuwepo”


Mchangiaji mwingine, Orvin Sanga akaandika “Mumsaidie huyo binti sasa kisaikolojia ku recover (kurejea katika hali yake ya kawaida) sio kazi rahisi lakini jitahidini”


Waziri Gwajima akamjibu kuwa “Hili linazingatiwa vema kupitia wataalamu wa ustawi wa jamii na wanasaikolojia. Ahsante sana kwa kujali”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad