P Diddy Aweka Posti ya Kwanza Instagram Tangu Akamatwe

 

P Diddy Aweka Posti ya Kwanza Instagram Tangu Akamatwe

Sean “Diddy” Combs alivunja ukimya wake wa mitandao ya kijamii Jumanne, Oktoba 15, aliporejea Instagram kumtakia binti yake, Love Sean Combs, heri ya siku ya kuzaliwa. Love Combs alitimiza miaka 2, na Diddy alichapisha picha kadhaa za tukio hilo, akionyesha binti yake akifurahia keki na kucheza na baba yake baharini.


"Happy Birthday @loveseancombs daddy loves you," aliandika kwenye ujumbe wake. Hata hivyo, sehemu ya komenti imezimwa kwenye posti hiyo, na bado haijulikani ni vipi lilipostiwa wakati Diddy yupo gerezani.


Diddy alikamatwa Septemba 16 jijini New York kwa mashtaka ya usafirishaji haramu wa binadamu na uhalifu wa utapeli. Amekana mashtaka hayo, huku wakili wake akiendelea kudai kuwa hana hatia. Diddy anatarajiwa kubaki gerezani hadi kesi yake itakapoanza Mei 2025.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad