Pamoja na Kufungwa ila Mbwana Samatta Leo Kaupiga Kweli Kweli....




Nadhani wote sasa tumeuona umuhimu wa MBWANA ALLY SAMATTA @samagoal77 kwenye kikosi cha Taifa Stars zile kelele ambazo tulimpigia kocha mkuu wa Taifa stars Hemed Seleman Moroco wakati alipomuacha kumuita SAMATTA kwenye timu ya Taifa kwenye mchezo dhidi ya Ethiopia nadhani mmeona maana yake tulichokuwa tunakimaanisha leo amefanya kazi kubwa sana kwenye hizi dakika 45 za kipindi cha kwanza.

SAMATTA ameifanya eneo la mstari wa mwisho wa ulinzi la DR Congo kukosa utulivu muda wote na kuhaha kila dakika kwa namna ambavyo alikuwa anatengeneza mashambulizi anatafuta nafasi anatengeneza nafasi na kulisogelea eneo la 14 zone la Congo.

Hii ndio faida ya kuwa na mchezaji professional wa Kimataifa anayecheza Ulaya wa aina yake SAMATTA hakwenda kucheza Ulaya kwa Bahati Mbaya tujaribu kuheshimu watu.

Salute Popa Captain diego🫡🫡🫡 @samagoal77

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad