"Nilivyokuwa Chadema tumeandamana sana na hata mara ya mwisho tumeandamana kutoka stand ya Magufuli mpaka Umoja wa Mataifa, mpaka mgongo uliuma, tulitembea kilomita 26 tukiishia tu kukunja ngumi, sasa mimi mpaka misuli ilikaza wakaamua kunipakia kwenye gari.
.... Lakini maandamano yanafanya kazi sana kama mkiwa mnaaminika na wananchi na wananchi waone sababu ya kuandamana. Tuliandamana Mbeya, Dar Es salaam, Mwanza na maeneo mengi lakini ninachoweza kusema ni kuwa mkishapoteza kuaminika hata muandamane vipi haiwezi kuleta tija yoyote na hata wakati naandamana nilikuwa najua kabisa tumepoteza imani ila niliandamana tu kwasababu ya uwajibikaji wa pamoja.Watu walikuwa wanatuona vituko kwasababu kama Dar Es salaam tupo Milioni saba ilikuaje tunaandamana watu 1000 tu hivi."- Mch.Peter Msigwa kwenye SiasaZetu