R. Kelly Akanusha Madai ya Kumnyanyasa Kingono Binti yake wa Kumzaa

 

R. Kelly Akanusha Madai ya Kumnyanyasa Kingono Binti yake wa Kumzaa

Siku chache baada ya binti wa Mwanamuziki R. Kelly kuanika wazi madai kwamba alikuwa akifanyiwa vitendo vya unyanyasaji wa kingono na baba yake mzazi akiwa na umri mdogo, mwanasheria wa R. Kelly ameibuka na kujibu madai hayo ya Buku Abi.


Kwa mujibu wa TMZ, Mwanasheria wa Kellys Bi. Jennifer Bonjean amekanusha madai hayo kwa kusema “Bw. Kelly kwa nguvu amekanusha madai haya. Aliyekuwa mke wake pia aliwahi kuja na tuhuma kama hizi miaka kadhaa iliyopita.


Baada ya kuchunguzwa na idara husika ya Watoto na Huduma za Familia, hakuna kilichokutwa kuwa na ukweli. Na hao waliotengeneza hii filamu popote walipo, hawakumfikia R. Kelly au timu yake pengine kukanusha.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad