Raia wa Afrika Kusini Wana Imani na Chris Brown, Licha ya Baadhi Kumpinga Kufanya Show

Raia wa Afrika Kusini Wana Imani na Chris Brown, Licha ya Baadhi Kumpinga Kufanya Show


Raia wa Afrika Kusini wamejitokeza kuunga mkono tamasha la Chris Brown nchini humo, wakikosoa kundi la wanawake lililoanzisha petition ya kumzuia msanii huyo kutumbuiza Desemba mwaka huu, licha ya tiketi za tamasha hilo kuuzwa zote. Wengi wanasisitiza kuwa #ChrisBrown alishalipa kwa makosa yake kupitia kifungo na kufanya huduma za jamii.


Aidha, mashabiki wamebainisha kuwa Chris Brown ametoa fursa kwa wanawake wawili wa Afrika Kusini, @tyla na #Naledii ambao wamefaidika kwa njia kubwa kutokana na ushirikiano na msanii huyo. Naledi alipokea malipo ya shilingi milioni 7.7 na amepewa credits kwenye albamu yake 11:11, jambo linalomuwezesha kupata mapato milele. Pia, Tyla alipata nafasi ya kufungua ziara ya kimataifa ya Chris Brown, hatua iliyokuza zaidi soko la muziki wake.


Mashariki wa Chris Brown wanakosoa ukimya uliopo kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mafanikio ya wanawake hawa wawili, huku wengine wakidai kundi linalopinga tamasha hilo lina upendeleo na linapaswa kuwaacha watu wachague wenyewe wanachotaka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad