Rais Samia Atoa Salamu za Pole Kwa Familia ya Dida

Rais Samia Atoa Salamu za Pole Kwa Familia ya Dida

Kufuatia kifo cha Mtangazaji wa Kipindi cha Mashamsham cha Wasafi Fm Khadija Shaibu maarufu kama Dida. Leo Rais Samia Suluhu Hassan @samia_suluhu_hassan ameonyesha kuguswa na msiba huo na kutoa salamu za pole kwa familia ya Dida, wafanyakazi wenzie pamoja na ndugu jamaa na marafiki.

Kupitia akaunti zake za mitandao ya kijamii Rais Samia amechapisha picha ya Dida huku akiandika ujumbe ufuatao "Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wafanyakazi wa Wasafi Media Group kwa kuondokewa na ndugu yetu, Khadija Shaibu (Dida). Mwenyezi Mungu mwingi wa rehma awape subra.

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.

Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa hakika kwake Yeye tutarejea"

Dida anatarajiwa kuzikwa leo saa kumi jioni katika makaburi ya Kisutu jijini Dar Es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad